MAXMALIPO YAZINDUA MFUMO WA UWEKAJI SALIO KWENYE KADI ZA MABASI YA MWENDO HARAKA KUPITIA KWA MAWAKALA WA MAXMALIPO

 Mkuu wa kitengo cha biashara Kampuni ya Maxmalipo Bw.Deogratius Lazari  Akifafanua Jambo kwa Waandishi wa habari na Kushoto ni Mkuu wa uendeshaji Kampuni ya Maxmalipo Bw. Ahmed Lussasi

Mkurugenzi Uendeshaji wa kampuni ya Maxmalipo (kulia) Bw. Ahmed Lussasi Akielezea Jinsi kampuni ilivyo piga hatua katika teknolojia, Kushoto ni Msemaji wa kampuni ya Uendeshaji wa Mabasi ya mwendo haraka Bw. Deus Bugaywa .

Msemaji wa Kampuni ya Undeshaji wa mabasi ya Mwendo haraka Bw. Deus Bugaywa (Kushoto)  Akifafanua Jambo kwa wanahabari na Kulia ni Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni ya Maxmalipo Bw.Ahmed LussasiKuanzia sasa wasafiri wenye kadi maalumu za Usafiri (Dart card) wameongezewa njia mbadala za kuweka salio katika kadi zao za Usafiri kwa kuwatumia mawakala wa Maxmalipo. Mteja mwenye kadi hii ya usafiri anaweza kufika kwa Wakala yeyote wa Maxmalipo na kuweka salio kiasi chochote kwenye kadi yake


Akiongea kwenye uzinduzi huu afisa Mwendesgaji mkuu wa Maxmalipo Bw. Ahmed Lussasi Amesema “ Lengo kubwa la kampuni ya Maxcom Africa imekua ni kujenga na kutengeneza mifumo imara na madhubuti ambayo inalenga kurahisisha ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki pia kusimamia na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato kwa kutumia mifumo ya Kielektroniki. Bw. Ahmed ameendelea kuelezea kwamba  Tangu Mradi huu wa Mwendo kasi umeanza  kumekua na maboresho mbalimbali na mbinu za kitaalamu zinazopelekea kukua kwa makusanyo, kuepusha na kudhibiti upotevu wa Mapato na kuhakikisha kuna uwazi wa hali ya juu katika utoaji wa taarifa za makusanyo (Real time Revenue reporting)”


Naye Msemaji wa kampuni ya undeshaji wa Mabasi haya ya Mwendokasi Bw. Deus Bugaywa  Ameelezea kwa Ufupi mafanikio kampuni iliyo yapata kwa kutumia mifumo hii ya kielektroniki moja ikiwa ni uhakika wa mapato, ukuaji wa mapato pamoja na usalama wa fedha zao”. Deus ameongeza kwa kusema “ Naweza kuwadhihirishia kwa ushirikiano huu tulio nao na Maxmalipo katika mradi huu umeleta Mageuzi makubwa katika sekta ya usafirishaji nchini kwetu barani Africa na Duniani kwa ujumla; Huu ndio mfumo pekee unaowezesha watu kuweka salio katika kadi zao kupitia MItandao ya simu na ndio mfumo Pekee uliokua kiteknolojia ndani ya muda mfupi Zaidi, na leo salio na ticket vinaweza kupatikana kwa mawakala waliopo hata mitaani (hawa wa Maxmalipo). Ni pongezi kwa Maxmalipo kama kampuni ya kitanzania kwa kufanya haya, lakini Zaidi Tutoe shukrani zetu kwa serikali kwa kuunga mkono Jitihada hizi katika sekta nzima ya usafiri.
Naye Mkuu wa Kitengo cha biashara katika kampuni ya Maxmalipo – Bw. Deogratius Lazari , amwewaambia wana habari kwamba Maxcom Africa ina Zaidi ya mawakala 15000 nchi nzima ambao wamewezeshwa kutoa huduma hii kwa watumiaji wa kadi hizi za mwendo haraka. Bw Deogratius ameainisha pia kwamba Mawakala hawa wa Maxmalipo wapo jirani na makazi ya watu hvyo wasafiri wanaweza kujipatia huduma hii kabla ya kufika kwnye vituo vya mabasi ya mwendo haraka.
Kufuatia Uzinduzi huu kampuni ya Maxcom Africa inatarajia kupungua kwa foleni za abiria kwnye vituo vya mabasi ya mwendo hasa wale wanaokua wakihitaji kuweka salio kwnye kadi zao pia wanataraji kuongezeka kwa Ajira katika sekta isiyo rasmi kwa watanzania wengi kuchamgamkia Fursa ya kuwa mawakala wa Maxmalipo ambayo itawaongezea kipato.


Maxcom Africa imekua ni Moja ya Kampuni za Kitanzania iliyofanikiwa sana katika uwekaji wa mifumo madhubuti ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato hapa Tanzania hasa katika miradi mikubwa ikiwamo huu wa mabasi ya Mwendo Kasi, TRA, Vivuko, Mahospitali (Moi)  na kwenye Kodi za halmashauri.