Tigo, serikali zasaini makubaliano kuunganisha shule za sekondari na intaneti


 Afisa Mkuu wa Kitengo cha Biashara kutoka Tigo, Shavkat Berdiev® na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu Pro. Faustine Kamuzora(L) wakisaini makubaliano kwa ajili ya kuunganisha kufikiwa kwa intaneti katika shule za sekondari nchini ili kuwezesha elimu kielektroniki shuleni katika hafla iliyofanyika mapema jana katika shule ya sekondari Jangwani Jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu Pro. Faustine Kamuzora akiongea na mmoja wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani mara baada ya kusaini saini makubaliano kwa ajili ya kuunganisha kufikiwa kwa intaneti katika shule za sekondari nchini ili kuwezesha elimu kielektroniki shuleni katika hafla iliyofanyika shuleni hapo mapema jana.

Dar es Salaam  Julai 13, 2016-kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imeingia ubia na Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu katika kuwezesha kufikiwa kwa intaneti katika shule za sekondari nchini  ili kuwezesha elimu kielektroniki shuleni  katika zoezi ambalo litachukua miaka miwili.

Kama sehemu ya makubaliano hayo, wizara itabainisha na kutoa orodha ya  shule zisizo na maabara za kompyuta ili ziunganishwe na hali kadhalika  kuongoza utekelezaji wa mradi  wakati Tigo itadhamini maendeleo ya miundombinu katika shule nchini ikiwa ni pamoja na kuunganisha nyaya ndani ya madarasa  na kufunga visivyotumia nyaya (LAN) na vituo vinavyofikia  mtandao wa intaneti.

 Alipokuwa akisaini makubaliano hayo katika Shule ya Sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam, Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev, alisema, “Kupitia Idara yetu ya huduma kwa jamii hivi sasa tunatekeleza  dira ya serikali  ya kuibadilisha nchi kuingia katika uchumi uliojikita katika uelewa ifikapo mwaka 2025 na kampuni yetu  imejipanga kuhakikisha  shule nyingi za sekondari Tanzania  zinafikiwa na mtandao wa intaneti.

 “Tunajivunia  kushirikiana na Wizara ya mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu  katika kuwezesha vijana  na jamii kwa ujumla  kuingia katika  mkondo wa kidunia wa habari  na uelewa, ambako watajifunza, kupanua uelewa wao na kushirikiana na wenzao katika sehemu mbalimbali duniani.”
Berdiev aliongeza kusema, “Tigo itaendelea  kufanya kazi na serikali  katika miradi  mingine ya ubunifu na inayovutia ili kunyanyua maisha ya Watanzania walio wengi”.

Akiishukuru Tigo wakati wa kusaini makubaliano hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu Pro. Faustine Kamuzora alisema, “Ni kupitia ushirikiano kama huu ndipo tutaweza kusambaza stadi za kisasa za Tehama pamoja na uelewa kwa vijana ili kuwawezesha  kukabiliana na changamoto  zinazotokana na mtiririko wa mabadiliko ya habari ya kila siku ndani ya jamii na katika uchumi wa dunia.”

Prof. Kamuzora aliongeza, “Naipongeza Tigo kwa utayari wake wa kujingiza katika makubaliano baina ya sekta binafasi na sekta za umma ili kuwasaidia wanafunzi wa shule za sekondari nchini Tanzania na vile vile tunakaribisha wadau wengine  kushiriki kuunganishwa kwa teknolojia hii.
Mradi wa kielektroniki mashuleni (eSchools) ni moja ya miradi mkakati ya uwekezaji kijamii ya Tigo na hadi sasa Tigo imeweza kuunganisha shule 31 za sekondari za serikali  na  mtandao wa intaneti ikiwa na mpango wa baadaye wa kuziunganisha  shule 50 kwa mwaka huu.