Tigo yazindua jukwaa la kujifunza la mtandao wa SMS kwa shule za sekondari


Mkurugenzi Mtendaji wa  Shule Direct, Faraja K. Nyalandu (wa kwanza kulia) Meneja wa Huduma za jamii wa Tigo  , Woinde Shishael(wa pili kulia), Mkuu wa Mfuko wa Human Development Innovation Fund (HDIF), David B. McGinty, (wa kwanza kushoto), Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika  mtihani wa kidato cha nnemwaka 2015/16 kutokea shule ya wavulana Fezza ya jijini Dar es Salaam, Innocent Lawrence (wa pili kushoto) na Mkurungezi wa Tume ya sayansi na teknolojia Flora Ismail Tibazarwa (wa tatukushoto)wakitazama namna mfumo wa huduma mpya ya wanafunzi kujifunza kupitia ujumbe mfupi wa maandishi, MAKINI SMS unavyoweza kufanya kazi kupitia simu ya mkononi

Wanafunzi i wa shule ya sekondari Azania na wageni waalikwa wakishuhudia uzinduzi wa  wa jukwaa  la kielimu  la SMS Makini ambalo litakuwa linatoa masuala mbalimbali ya kijifunza  kupitia mtandao  kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari nchini mapema mwishoni mwa wiki iliyopita ,Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika shule ya sekondari Azania Jijini Dar es salaam. 


Meneja wa Huduma za jamii wa Tigo  , Woinde Shishael (Wa kwanza kulia ) akizungumza na waandishi wa habari ,Pembeni yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa  Shule Direct, Faraja K. Nyalandu mara baada ya uzinduzi  wa jukwaa  la kielimu  la SMS Makini ambalo litakuwa linatoa masuala mbalimbali ya kujifunza  kupitia mtandao  kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari nchini mapema mwishoni mwa wiki iliyopita ,Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika shule ya sekondari Azania Jijini Dar es salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa  Shule Direct, Faraja K. Nyalandu akizungumza na vyombo mara baada ya mara baada ya uzinduzi  wa jukwaa  la kielimu  la SMS Makini ambalo litakuwa linatoa masuala mbalimbali ya kijifunza  kupitia mtandao  kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari nchini mapema mwishoni mwa wiki iliyopita ,Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika shule ya sekondari Azania Jijini Dar es salaam. Wanafunzi wa shule ya sekondari Azania ya jijini Dar es Salaam wakielekezana namna ya kutumia  jukwaa  la kielimu  la SMS Makini ambalo litakuwa linatoa masuala mbalimbali ya kijifunza  kupitia mtandao  kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari nchini mapema mwishoni mwa wiki iliyopita ,Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika shule ya sekondari Azania Jijini Dar es salaam.

Kampuni  inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania  kwa kushirikiana na asasi ya ndani inayofanya ujasiriamali kwa njia  ya mtandao, Shule Direct  imezindua  jukwaa  la kielimu  la SMS Makini ambalo litakuwa linatoa masuala mbalimbali ya kijifunza  kupitia mtandao  kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari nchini.
Meneja wa Huduma za jamii wa Tigo  , Woinde Shishael alisema wakati wa hafla  ya uzinduzi huo kwenye Shule ya Sekondari Azania jijini Dar es Salaam leo kwamba SMS Makini zitawawezesha wanafunzi  kuzifikia zana za kujifunza kidijitali  kupitia mtandao na hivyo kuziba pengo lililopo  la rasilimali za kujifunzia  kwenye sekta ya elimu.
“Kupitia  matumizi ya SMS Makini watumiaji wa Tigo, na hususan wanafunzi na walimu wa shule za sekondari wataweza kuipata miuhtasari ya kidijitali, mafunzo, mazoezi, kupata maelezo pamoja na video moja kwa moja kupitia simu ya mkononi,” alisema Woinde.
Alieleza kwamba madarasa yatakayohusishwa  kwenye jukwaa hilo ni kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne  na kuongeza kuwa maelezo ya mafunzo yatakuwa yanazingatia mtaala wa elimu wa Tanzania ukihusisha masomo tisa.
Masomo hayo ni pamoja na Historia, Uraia, Jiografia. Fizikia, Kemia, Kiingereza, Hisabati na Kiswahili.
Kwa mujibu wa Woinde SMS Makini za Tigo pia zitawaunganisha walimu na wanafunzi na fursa ya kujadiliana, kushirikishana mawazo, kurejea, na kupakua mitihani iliyopita ya Baraza la Mitihani la Taifa na hali kadhalika kuwasiliana kwenye mtandao na wanafunzi 10,000 waliosajiliwa.
Wateja wa Tigo wataweza kuipata huduma hiyo bure kwa mwezi mmoja na baada ya hapo watakuwa wanatozwa ada ya siku ya shilingi 100 na ada ya  wiki ya shilingi 500, alisema Woinde.
Kuipata huduma hiyo  wateja wa Tigo wanatakiwa kutuma  neno ‘Makini’ kwenda namba 15397 na baadaye kufuata maelekezo yatakayokuwa yanatolewa.
Ushirikiano na asasi ya Shule Direct ni sehemu ya mkakati wa Tigo wa kuunga mkono miradi ambayo ina manufaa makubwa ndani ya jamii.
          mwisho  –